TUTAFAKARI VIJANA NA
UKOSEFU WA AJIRA.
DEOGRATIAS MUTUNGI.
Kwa sasa hali ni tete na ya kutisha sana katika
suala la ajira hapa nchini, vijana wanasaga meno na kulia wazazi na walezi
wananungunika na serikali ina haa na
kutapatapa kutatua janga hili bila mafanikio ya kuridhisha, hapa kwetu
Tanzania ajira ni kama janga la kitaifa
kwa sasa kama yalivyo majanga mengine,
ya njaa, tsunami, ukimwi, kansa na kisukari, japo serikali haikubali hilo kwa
kutaka kulinda dola lake na kutotaka kuonyesha kuwa kweli imelemewa, dhaifu na imeshindwa kutimiza kile ilicho kihaidi kupitia ilani yake wakati wa
kinyanganyiro cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2005/ 2010.
Ni wazi kuwa serikali imeshindwa kuja na mbinu
mbadala za kupambana na janga hili, ambalo kwa sasa uwiano wa vijana
wanaowezeshwa kupata ajira serikalini ni asilimia ndogo sana ukilinganisha na
kundi la wahitimu kutoka kwenye vyuo vikuu vyetu wanaohachwa njia panda bila kupatiwa ufumbuzi wa maisha yao licha ya
misukosuko, karaha na kuangaika kwao takribani miaka mitatu mpaka mitano
wanapokuwa chuoni wakijaribu kupata maarifa (Knowledge/ skills) ya kulitumikia taifa lao na badala yake
wamekuwa wakiachwa “solemba”
Kwa sasa vijana wamekata tamaa na ukosefu wa ajira
wanaisema vibaya serikali yao kwa kushindwa kupata mbinu mbadala za kupambana
na janga hili la ajira ambalo kimantiki
na kimtazamo wa mbali (long sight) ni
janga hatari ambalo kwa hualisia wake linaweza kusababisha madhara makubwa ya
kisiasa na kupelekea uvunjifu wa amani kama ambavyo tumeweza kushuhudia kwa
wenzetu wa kaskazini hasa Tunisia ambapo kiini kikubwa cha mapinduzi ya nchi ya
Tunisia ni chembechembe za ajira ambapo kijana mmoja mhitimu wa chuo kikuu
aliyekosa ajira kwa muda mrefu kuamua kujilipua kwa moto tena mbele ya jengo la wizara ya
ajira na kazi ya nchini humo.
Uamuzi huo ulifikiwa na kijana huyu baada ya kuona
serikali yake imekosa sera mbadala za ufumbuzi wa suala la ajira ambapo kwa
wakati huo lilikuwa ni janga kwa vijana walio wengi nchini humo hasa wale wenye
kisomo cha chuo kikuu.
Je? Ni nini kilifuata Tunis kama sio mapinduzi ya umma yaliyoenda sambamba
na kungolewa kwa rais wa nchi hiyo bwana
Zine El bidine beni ali aliyeweza
kukomaa madarakani takribani miaka 23, tokea mwaka 1987.
Ni viongozi wachache walioweza kusimama kidete na
kukili hadharani kuwa ili ni janga na bomu linalokaribia kulipuka, na mushukru
mheshimiwa Edward Lowasa aliliona hilo na kulisemea wazi bila kumungunya
maneno.
Lakini si wote walio na ujasiri
kama wa Lowasa, wengi wao wameshindwa
kujibu na kubainisha ukweli wa hoja juu
ya chanzo kikuu cha ukosefu wa ajira hapa nchini ni nini? na badala yake wamekuwa wakitumia majukwaa ya
siasa kuraghai na kupotosha ukweli wa
jambo hili na wengi wao wamekuwa wanafiki wa kimtazamo juu ya suala hili ambapo
wamekuwa wakiliminya na ili lionekane ni jambo tu la kawaida, ukweli wa mambo ni kuwa sasa ajira ni
ombwe (Vaccum) linaloitaji ufumbuzi na mjadala wa kitaifa, ni asilimia 13.4 ya vijana wasiokuwa na ajira
hapa nchini takwimu kutoka mamlaka za serikali ambazo bado wadau wa takwimu
wanapingana nazo kwa madai kuwa hizo ni asilimia ndogo kulinganisha na tatizo
lenyewe lilivyo kwa sasa.
Je viongozi wetu wanaienzi vipi sera ya taifa ya
vijana iliyochini ya wizara ya kazi na
maenedeleo ya vijana ya mwaka 1977 na ile iliyofanyiwa marekebisho mwaka 1984 ,
1995 na 1996 sera hii inabainisha wazi umuhimu wa kijana katika jamii na
inaelekeza serikali kutekeleza wajibu wake kwa kundi hili ambalo linaonekana
kuwa kubwa na linalo ongezeka kila kukicha.
Katika sSura ya pili ya sera ya taifa ya vijana
katika utangulizi wake wa ‘’UMUHIMU WA SERA YA MAENDELEO YA VIJANA”Katika
kipengele cha 2.2.1 kinabainisha wazi kuwa ni jukumu la serikali kutambua
matatizo ya vijana na taifa lao. Na kipengele cha pili 2.2.2, kinasema wazi
kuwa ni jukumu la serikali kutambua uwezo
wa vijana na wajibu wao katika kuchangia maendeleo ya taifa, nacho
kipengele cha tatu 2.2.3, kinasema wazi kuwa ni jukumu la serikali kubainisha
na kutumia rasilimali zilizopo katika mazingira yao.
Swali ni je? Wenye dhamana wanatimiza vipi sera
hizo? Au waliopewa dhamana ya
kuhakikisha vijana wanapatiwa fursa za ajira wanatimiza wajibu wao ipasavyo au
wapowapo tu mbumbu wanaotumia mamlaka kwa misingi ya udhalimu na ufisadi kwa
maslahi yao na familia zao.
Ni jukumu la viongozi wetu akiwemo rais wa
nchi hii kutafakari kwa kina suala hili la ukosefu wa ajira kwa vijana ni kwa
jinsi gani wataweza kulitatua na hatimaye kulipatia ufumbuzi na wakudumu maana
janga la ajira kwa vijana ni kama bomu ambalo limetegwa sehemu na linaloweza
kulipuka wakati wowote na kwa kawaida madhara haya uwa ni makubwa kuliko wao
wanavyofikri, ingekuwa vema kama viongozi wetu wangekuwa watu wa kusoma alama
za nyakati bila kubweteka na kujiona wao
wamefika hapo walipo , eti kwa sababu suala la ajira kwa familia zao na koo zao
sio ombwe wala tatizo tena kwao kutokana na mtandao “ Network” ambao tayari wameisha ujenga.
Je? Siku mtandao huo ukitibuliwa na vijana hao ambao
ndio nguvu ya umma nini kitafuata kama
si yale ya akina Zine El bidine beni ali
na yale ya Hussen Mubarack wa misri. Ni vema serikali yetu ikatambua kuwa inao uwezo
mkubwa wa kukabiliana na janga hili la ajira kwa vijana kabla alijalipuka kwa kutumia rasilimali
zetu kwa kujenga nyenzo za ajira kama viwanda
vidogovidogo, mikopo ya kibiashara kwa vijana yenye riba nafuu na utoaji wa
elimu hasa somo la ujasiriamali kwa vijana ili kuweza kuelewa jinsi ya kufanya
biashara kiutalaamu.
Vi vema viongozi wetu watafakari suala hili kwa
umakini zaidi na watambue nguvu na ushawishi mkubwa uliopo ndani ya kundi hili,
kundi hili ni hatari na halipaswi kuchezewa shere kama wanavyofanya viongozi wa
sasa ambao wao wanaridhika na nafasi zao walizo nazo leo bila kujua hatima ya
kesho kasumba ambayo inawagharimu viongozi wengi wa Afrika ambao mara nyingi
huishia pabaya, historia inawahukumu na iko wazi bila kificho, viongozi wenye
mamlaka wajue kuwa kuna usemi usemao “ Unemployment is the parent of revolution
and crime”
Waziri wa kazi na ajira Mheshimwa Gaudensia Mugosi
Kabaka