Wednesday, January 28, 2015



                    TUTAFAKARI VIJANA NA UKOSEFU WA AJIRA.

DEOGRATIAS MUTUNGI.

Kwa sasa hali ni tete na ya kutisha sana katika suala la ajira hapa nchini, vijana wanasaga meno na kulia wazazi na walezi wananungunika  na serikali ina haa na kutapatapa kutatua janga hili bila mafanikio ya kuridhisha, hapa kwetu Tanzania  ajira ni kama janga la kitaifa kwa sasa  kama yalivyo majanga mengine, ya njaa, tsunami, ukimwi, kansa na kisukari, japo serikali haikubali hilo kwa kutaka kulinda dola lake na kutotaka kuonyesha kuwa kweli imelemewa,  dhaifu na imeshindwa kutimiza kile  ilicho kihaidi kupitia ilani yake wakati wa kinyanganyiro cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2005/ 2010. 

Ni wazi kuwa serikali imeshindwa kuja na mbinu mbadala za kupambana na janga hili, ambalo kwa sasa uwiano wa vijana wanaowezeshwa kupata ajira serikalini ni asilimia ndogo sana ukilinganisha na kundi la wahitimu kutoka kwenye vyuo vikuu vyetu wanaohachwa njia panda  bila kupatiwa ufumbuzi wa maisha yao licha ya misukosuko, karaha na kuangaika kwao takribani miaka mitatu mpaka mitano wanapokuwa chuoni wakijaribu kupata maarifa (Knowledge/ skills)  ya kulitumikia taifa lao na badala yake wamekuwa wakiachwa “solemba”

Kwa sasa vijana wamekata tamaa na ukosefu wa ajira wanaisema vibaya serikali yao kwa kushindwa kupata mbinu mbadala za kupambana na janga hili  la ajira ambalo kimantiki na kimtazamo wa mbali (long sight)  ni janga hatari ambalo kwa hualisia wake linaweza kusababisha madhara makubwa ya kisiasa na kupelekea uvunjifu wa amani kama ambavyo tumeweza kushuhudia kwa wenzetu wa kaskazini hasa Tunisia ambapo kiini kikubwa cha mapinduzi ya nchi ya Tunisia ni chembechembe za ajira ambapo kijana mmoja mhitimu wa chuo kikuu aliyekosa ajira kwa muda mrefu kuamua kujilipua  kwa moto tena mbele ya jengo la wizara ya ajira na kazi ya nchini humo.

Uamuzi huo ulifikiwa na kijana huyu baada ya kuona serikali yake imekosa sera mbadala za ufumbuzi wa suala la ajira ambapo kwa wakati huo lilikuwa ni janga kwa vijana walio wengi nchini humo hasa wale wenye kisomo cha chuo kikuu.
Je? Ni nini kilifuata Tunis  kama sio mapinduzi ya umma yaliyoenda sambamba na kungolewa kwa  rais wa nchi hiyo bwana Zine El bidine beni ali  aliyeweza kukomaa madarakani takribani miaka 23, tokea mwaka 1987.

Ni viongozi wachache walioweza kusimama kidete na kukili hadharani kuwa ili ni janga na bomu linalokaribia kulipuka, na mushukru mheshimiwa Edward Lowasa aliliona hilo na kulisemea wazi bila kumungunya maneno.

Lakini si wote walio na ujasiri kama wa Lowasa, wengi wao  wameshindwa kujibu na kubainisha ukweli wa hoja  juu ya chanzo kikuu cha ukosefu wa ajira hapa nchini ni nini?  na badala yake wamekuwa wakitumia majukwaa ya siasa kuraghai na kupotosha  ukweli wa jambo hili na wengi wao wamekuwa wanafiki wa kimtazamo juu ya suala hili ambapo wamekuwa wakiliminya na ili lionekane ni jambo tu la kawaida, ukweli wa  mambo ni  kuwa  sasa ajira ni  ombwe (Vaccum) linaloitaji ufumbuzi na mjadala wa kitaifa, ni  asilimia 13.4 ya vijana wasiokuwa na ajira hapa nchini takwimu kutoka mamlaka za serikali ambazo bado wadau wa takwimu wanapingana nazo kwa madai kuwa hizo ni asilimia ndogo kulinganisha na tatizo lenyewe lilivyo kwa sasa.

Je viongozi wetu wanaienzi vipi sera ya taifa ya vijana iliyochini ya wizara ya  kazi na maenedeleo ya vijana ya mwaka 1977 na ile iliyofanyiwa marekebisho mwaka 1984 , 1995 na 1996 sera hii inabainisha wazi umuhimu wa kijana katika jamii na inaelekeza serikali kutekeleza wajibu wake kwa kundi hili ambalo linaonekana kuwa kubwa na linalo ongezeka kila kukicha.
Katika sSura ya pili ya sera ya taifa ya vijana katika utangulizi wake wa ‘’UMUHIMU WA SERA YA MAENDELEO YA VIJANA”Katika kipengele cha 2.2.1 kinabainisha wazi kuwa ni jukumu la serikali kutambua matatizo ya vijana na taifa lao. Na kipengele cha pili 2.2.2, kinasema wazi kuwa ni jukumu la serikali kutambua uwezo  wa vijana na wajibu wao katika kuchangia maendeleo ya taifa, nacho kipengele cha tatu 2.2.3, kinasema wazi kuwa ni jukumu la serikali kubainisha na kutumia rasilimali zilizopo katika mazingira yao. 

Swali ni je? Wenye dhamana wanatimiza vipi sera hizo?  Au waliopewa dhamana ya kuhakikisha vijana wanapatiwa fursa za ajira wanatimiza wajibu wao ipasavyo au wapowapo tu mbumbu wanaotumia mamlaka kwa misingi ya udhalimu na ufisadi kwa maslahi yao na familia zao.

   Ni jukumu la viongozi wetu akiwemo rais wa nchi hii kutafakari kwa kina suala hili la ukosefu wa ajira kwa vijana ni kwa jinsi gani wataweza kulitatua na hatimaye kulipatia ufumbuzi na wakudumu maana janga la ajira kwa vijana ni kama bomu ambalo limetegwa sehemu na linaloweza kulipuka wakati wowote na kwa kawaida madhara haya uwa ni makubwa kuliko wao wanavyofikri, ingekuwa vema kama viongozi wetu wangekuwa watu wa kusoma alama za nyakati  bila kubweteka na kujiona wao wamefika hapo walipo , eti kwa sababu suala la ajira kwa familia zao na koo zao sio ombwe wala tatizo tena kwao kutokana na mtandao  “ Network” ambao tayari wameisha ujenga. 

Je? Siku mtandao huo ukitibuliwa na vijana hao ambao ndio  nguvu ya umma nini kitafuata kama si yale ya akina  Zine El bidine beni ali na yale ya Hussen Mubarack wa misri. Ni vema serikali yetu ikatambua kuwa inao uwezo mkubwa wa kukabiliana na janga hili la ajira kwa vijana  kabla alijalipuka kwa kutumia rasilimali zetu  kwa kujenga nyenzo za ajira kama viwanda vidogovidogo, mikopo ya kibiashara kwa vijana yenye riba nafuu na utoaji wa elimu hasa somo la ujasiriamali kwa vijana ili kuweza kuelewa jinsi ya kufanya biashara kiutalaamu.

Vi vema viongozi wetu watafakari suala hili kwa umakini zaidi na watambue nguvu na ushawishi mkubwa uliopo ndani ya kundi hili, kundi hili ni hatari na halipaswi kuchezewa shere kama wanavyofanya viongozi wa sasa ambao wao wanaridhika na nafasi zao walizo nazo leo bila kujua hatima ya kesho kasumba ambayo inawagharimu viongozi wengi wa Afrika ambao mara nyingi huishia pabaya, historia inawahukumu na iko wazi bila kificho, viongozi wenye mamlaka wajue kuwa kuna usemi usemao “ Unemployment is the parent of revolution and crime”





Waziri wa kazi na ajira Mheshimwa Gaudensia Mugosi Kabaka








                                                                                         

 

No comments:

Post a Comment